KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amefunguka kuwa kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Simba watamkosa straika wao mpya, Lazarious Kambole.

Akizungumzia maandalizi yao, Nabi amesema “Tunashukuru tupo sawa kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Simba.

yanga, Yanga Kumkosa Lazarious Kambole, Meridianbet

“Tumekuwa na maandalizi kwa muda mfupi lakini tumejitahidi kuendana na muda ila kikubwa tumejiandaa vizuri na tunatambua umuhimu wa mchezo huu kwamba unaangaliwa na nchi nyingi Afrika hivyo tuna imani tunaenda kupata matokeo.

“Tutamkosa Kambole kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini kwa upande wa Jesus Moloko yeye tayari ameanza mazoezi na timu hivyo atakuwa sehemu ya kikosi.

“Kwenye mchezo dhidi ya Vipers tulikuwa hatujajiandaa vizuri kutokana na muda ambao tuliingia kambini tofauti na Vipers lakini nilipata picha halisi ya kikosi changu na haikuwa lazima tupate matokeo katika ule mchezo.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa