Simba Kuwapa Majukumu Wachezaji Wake

KOCHA Mkuu wa Simba, Zoran Maki amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga anatarajia wachezaji waliopo kwenye kikosi watampa matokeo mazuri.

Mchezo huo wa Ngao ya jamii utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo utakuwa maalum kwa ajili ya kufungua pazia la ligi kuu kwa msimu wa 2022/23.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Maki amesema: “Tumeendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga na hakuna kipya zaidi katika mazoezi lakini kitu cha muhimu zaidi kwa wachezaji ni kujua umuhimu wa mchezo.

“Utakuwa mchezo mgumu sana pia wa nguvu ila nina imani kwamba wachezaji wangu watajiandaa vyema na kufanya vizuri katika mchezo huo mkubwa na tutapata matokeo mazuri.

“Siku zote mashabiki wanapenda kushinda lakini utakuwa mchezo mgumu ila hauwezi kuwa mgumu kwenye taaluma yangu kutokana na sehemu ambazo nilizowahi kufundisha.”

Acha ujumbe