Simba juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa walitangaza rasmi majembe yao mapya na benchi lote la ufundi kuelekea msimu ujao wa 2022/23 huku pia wakitoa burudani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya ST. George ya Ethiopia.

Jumamosi hii Simba wanatarajiwa kuvaana na Yanga katika mchezo wa ufunguzi wa ligi maarufu mchezo wa Ngao ya Jamii, unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Barbara alisema: “Kwa niaba ya uongozi tunashukuru kwa sapoti kubwa ambayo mashabiki wetu wamekuwa wakituonyesha siku zote, lakini hasa katika tamasha letu la Simba Day.
“Najivunia ubora ulioonyeshwa na kikosi chetu, nadhani kila mmoja ameona ubora mkubwa wa watu tuliowasajili, hii ina maana kuwa tumejipanga kufanya makubwa msimu ujao, kwa sasa tumesahau kuhusiana na kile kilichotokea Jumatatu na nguvu yetu kubwa ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa Jumamosi dhidi ya Yanga.”

