IKIWA kesho Coastal Union watakwenda kukutana na Yanga kwenye mchezo wao wa pili wa ligi kuu dhidi ya Yanga, kocha wa timu hiyo Juma Mgunda amekiri kuwa wapinzani wao wako bora kwenye kila eneo na wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuweza kupata ushindi.

Mgunda alifunguka kuwa Yanga wamekuwa bora sana kwa sasa kwa kuwa wana timu ambayo ina benchi bora la ufundi na imetoka kushinda kwenye mechi mbili muhimu na mfululizo hivyo yeye na vijana wake wanatakiwa kuwa makini na kupambana hadi mwisho.

yanga, Mgunda: Yanga Wana Kila Kitu Kizuri Kwenye Timu Yao, Meridianbet

Akizungumzia mchezo huo Mgunda alisema: “Mchezo utakuwa mgumu sana, mimi na vijana wangu tunalijua hilo, kwa sababu tunakwenda kucheza na timu ambayo imetimia, ikiwa na wachezaji bora na benchi bora la ufundi.

“Hakuna kingine ambacho tunatakiwa kufanya zaidi ya kupambana kwa kila namna ili kuweza kutafuta matokeo ya ushindi.”

Huu ni mchezo wa pili kwa Coastal Union, mchezo wao wa kwanza walicheza na KMC na kuvuna ushindi wa bao 1-0. Yanga wao wakiwa Shekh Amri Abeid Arusha ambapo watacheza ten ana Coastal leo walishinda 2-1.

Mara ya mwisho Coastal na Yanga kukutana ilikuwa kwenye uwanja huo, Yanga wakishindakwa penalty 4-1 kweye mechi ya fainali ya FA ambayo dakika 90 ilimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa