KLABU ya Simba Queens itakuwa na dakika 90 leo kwenye muendelezo wa Mashindano ya Kanda ya Cecafa, mchezo ambao utawahakikishia kuvuka kwenda hatua ya nusu fainali kwa kufikisha alama tisa kwenye kundi A.

Simba walishinda mechi zao zote mbili za mwanzo kwa jumla ya mabao nane na leo wanatakiwa kuvuna alama watatu au hata moja ili waende zao kwenye nusu fainali ambapo kuna dalili zinonyesha huenda wakavaana na As Kigali ya Rwanda.

Simba, Simba Queens Kibaruani Tena Cecafa, Meridianbet

Wakati Simba wakipeta, wawakilishi wengine wa Tanzania, Warriors Queens kutoka Zanzibar wao walishindwa kuvuka kwenye alama ya makundi baada ya kuchapwa kwenye mech izote mbili kwa jumla ya mabao 12.

C.B.E ya Ethiopia, As Kigali, She Corpote na Simba ndiyo timu ambazo zinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kwenda nusu fainali.

Mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kusaka timu moja ambayo itawakilisha kanda ya Cecafa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa