KLABU ya Kagera Sugar imejiandaa vizuri kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara utakaochezwa kesho Agosti 20 dhidi ya Simba katika uwanja wa Mkapa Dar.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jana Ijumaa Makao Makuu ya TFF, yaliyopo Ilala Dar, kocha mkuu, Francis Baraza wao wamejipanga vizuri kuwakabili Simba ingawa haitakuwa rahisi kupata matokeo mazuri.

SIMBA, Kagera Maji ya Shingo kwa Simba, Meridianbet

“Kwa sasa tumejipanga vizuri kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Simba na tunatarajia matokeo mazuri.

“Japokuwa Simba ni timu kubwa na imechukua ubingwa zaidi ya mara moja, sisi tumejipanga vizuri na hata ukiangalia mchezo uliopita dhidi ya Azam FC, utaona jinsi tulivyojipanga na tutafika mbali.” Alisema.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa