BAADA ya kufungiwa kwa uwanja wao wa Highland Estates, Uongozi wa Ihefu umefunguka kuwa watarejea kwenye Uwanja wao kukipiga na Yanga.

Ihefu wanatarajia kucheza mechi yao ya pili ya ligi kuu kesho dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar baada ya kufungiwa kwa uwanja wao. Kikosi hicho chini ya Kocha Mkuu, Zubeir Katwila kinatarajia kucheza mechi yao kwenye Uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Yanga, Septemba 29, mwaka huu.

Ihefu

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew amesema kuwa: “Maandalizi yamekamilika kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Namungo. 

“Itatuathiri kwa namna moja ama nyingine kucheza kwenye Uwanja mpya lakini tunaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo kwenye mchezo huo baada ya kupoteza ule wa kwanza. 

“Tutarejea kwenye Uwanja wetu wa nyumbani baada ya mapumziko ya wiki mbili hivyo kila kitu kitakuwa sawa na mashabiki wetu wa mbarali watatuona kwenye mchezo dhidi ya Yanga kwani tuna michezo miwili ya ugenini.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa