GOLIKIPA wa zamani wa Yanga, Ramadhan Kabwili amesaini mkataba wa kukitumikia kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda. 

Kabwili alikitumikia kikosi cha Yanga kwa mafanikio makubwa ambapo alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa akitokea kikosi cha vijana U20.

Kabwili, Kabwili Kuonekana Rwanda, Meridianbet

Kipa huyo anakumbukwa zaidi baada ya kucheza mechi ya dabi ya kariakoo dhidi ya Simba msimu wa 2019/20 ambapo alionyesha kiwango kikubwa licha ya timu hiyo kupoteza kwa bao 1-0.

Bao la mchezo huo lilifungwa na Meddie Kagere ambaye aliunganisha krosi kutoka kwa John Bocco.

Lakini kuanzia msimu wa 2020/21 mpaka kuondoka kwake mambo yalikuwa magumu kwa kipa huyo baada ya maingizo mapya ya makipa ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni Metacha Mnata na Faroukh Shikhalo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa