Klabu ya Yanga imeanza safari hii leo ya kuelekea jijini Tanga kwaajili ya kukipiga kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam ambao umepangwa kupigwa katika dimba la Mkwakwani.

Azam wao walishatangulia wakiwasubiri Yanga ambao bado wlaikuwa jijini Dar es salaam kusherehekea Ubingwa wao wa pili mfululizo ambao wameupata msimu huu ikiwa ni kombe la 29.
Kila timu inahitaji kupata kombe hilo ili kujiongezea mataji mengi ambayo wanayo mpaka sasa, huku kuna taarifa zikisema kuwa klabu hiyo ya Wananchi watawakosa wachezaji wao Mayele pamoja Aziz Ki.

Yanga ndio bingwa mtetezi wa ligi hadi sasa akijikusanyia pointi zao 78 huku Wanalamba lamba wao wakipata pointi zao 59 pekee kwenye michezo 30 ambayo wamecheza hadi ligi kumalizika.
Mechi ya mwisho kukutana, vijana wa Nabi waliondoka na ushindi na kesho vijana wa Chamazi wanasema wanataka kumfunga kama walivyomfunga pacha wake.

