Klabu ya Yanga imetua jijini Dar es salaam wakitokea Mbeya huku wakisindikizwa na sherehe za kutwaa Kombe la 29 la Ligi kuu ya NBC ambalo walikabidhiwa hapo jana baada ya ligi kumalizika.

Yanga walimaliza msimu jana kwa ushindi dhidi ya Tanzania Prisons ambao waliwapasua kwa mabao 2-0, mabao ya Fiston Mayele pamoja na Yanick Bangala yalitosha kuwapatia pointi 3.
Baada ya mechi hiyo kukamilika kule Mbeya klabu hiyo ambayo inaongozwa na Kocha mkuu Nabi walikabidhiwa kombe lao huku wakitangaza kufanya gwaride wakirejea nyumbani.

Na ndicho klinachofanyika toka asubuhi wakitembea na kombe lao karibu jiji zima wakiwa pamoja na mashabiki zao, huku wakiwa pia kwenye fainali ya Kombe la FA ambalo watamenyana dhidi ya Azam FC kule Tanga.

