Azam Yatangulia Tanga Kuwasubiri Yanga Kwaajili ya Fainali ya FA

Klabu ya Azam FC baada ya kumaliza ligi kibabe kwa kuitandika Polisi Tanzania mabao 8-0 jana, leo hii wameanza safari ya kuelekea Tanga ambapo itapigwa fainali ya Kombe la FA.

 

Azam Yatangulia Tanga Kuwasubiri Yanga Kwaajili ya Fainali ya FA

Azam FC waliingia hatua hii ya fainali kwa kuitoa Simba kwa mabao 2-1 na kujikatia tiketi moja kwa moja ya kucheza fainali huku Yanga wao walimtoa Singida Big Stars.

Wanalamba lamba wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi zao 59 ambapo watashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.

Wakati mabingwa wa ligi mara ya pili mfululizo Wananchi wao wamemaliza ligi wakiwa na pointi zao 78, na watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika  msimu ujao huku msimu huu wakiweka rekodi ya kufika Fainali Kombe la Shirikisho CAF.

Azam Yatangulia Tanga Kuwasubiri Yanga Kwaajili ya Fainali ya FA

Mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye ligi, vijana wa Chamazi walipoteza mchezo huo. Je fainali ya Jumapili wanaweza kulipa kisasi huku kukiwa na ongezeko la Feisali Salum?

 

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.