DODOMA Jiji wanatarajia kuzindua jezi zao mpya za msimu wa 2022/23 wikiendi hii ambazo zinatoka nchini Hispania. 

Akizungumzia matokeo yao, Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa: “Mchezo ulikuwa wa wazi kabisa na magoli ambayo tumefungwa yalikuwa ya halali kabisa.

Dodoma Jiji, Dodoma Jiji na Jezi za Hispania Msimu wa 2022/23, Meridianbet

Kiukweli Mbeya City walituzidi mbinu kwani baada ya kufunga bao la kwanza tulipumzika lakini wenzetu hawakuwa wamemaliza mechi ndio maana wakatuadhibu. 

“Kwa sasa tunaenda kutafuta furaha ya mashabiki wetu kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons ndio utakuwa mchezo wa kuadhibu. 

“Tunatarajia kupokea jezi zetu mpya kati ya jumamosi au jumapili kutoka Hispania, hivyo tunaenda kushinda ili kuhakikisha mashabiki wetu wanaona fahari ya kuvaa jezi zetu mpya.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa