MFUNGAJI wa bao pekee la Kagera Sugar, kwenye mchezo dhidi ya Azam, Anuary Jabir amefunguka kuwa matokeo ya mchezo huo wameyaacha na kwa sasa wanaangalia mchezo wao unaofuata dhidi ya Simba. 

Kagera Sugar walipoteza mchezo huo wa kwanza kwenye ligi mbele ya Azam FC kwa mabao 2-1 mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

SIMBA, Anuary Jabir: Simba wasubiri Moto Tu, Meridianbet

Mchezo wao unaofuata utakuwa dhidi ya Simba utakaopigwa Agosti 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Anuary amesema kuwa: “Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kumaliza mchezo salama, Azam ni timu nzuri tuliingia kwa kuiheshimu ili mradi tuweze kupata matokeo.

“Nashukuru msimu uliopita nilikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walifanya vizuri lakini msimu huu mipango yangu ni kuhakikisha nafanya vizuri zaidi.

“Benchi la ufundi limeona ni makosa gani ambayo tuliyoyafanya kwenye mchezo wa jana hivyo hatufikirii hilo bali tunaenda kufanya vizuri katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa