Simba Wawapa Matumaini Mashabiki

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa, wanatakiwa kusahau matokeo ya Kariakoo Dabi na badala yake wajipange kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu Bara, kwani bado wana kikosi imara.

Bosi huyo ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutoka kufungwa 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 “Wanasimba tumepoteza Kariakoo Dabi, hayakuwa malengo yetu msimu huu, hivyo tutulie na tuungane kwa pamoja tukianza msimu mpya ambao ninaamini unakwenda kuwa mzuri kwetu.

“Kama uongozi tunaamini haitakuwa rahisi kusahau, lakini tunapaswa kujisahaulisha maana ligi ndio inaanza, kikubwa tuwaachie kazi benchi la ufundi kwani wao ndio wanatengeneza timu ya ushindi, uzuri ni kwamba tayari wameona upungufu uliopo, hivyo watafanyia kazi yote.”

Makala iliyopita

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.