NYOTA wapya wa kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2022/23 wameliamsha kwa kufanya kweli katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Aziz ki
Aziz ki
Ni Bernard Morrison ambaye amerejea katika kikosi hicho akitokea Simba pamoja na Aziz KI ambaye alijiunga na Yanga akitokea kikosi cha ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Wawili hao kwa mbele ya Polisi Tanzania ubao uliposoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga kila mmoja aliweza kutoa pasi moja ya bao kwa kutumia mguu wa kulia.

Ni Aziz KI alifungua akaunti yake ya pasi ya bao kwa kumpa Fiston Mayele dk ya 41 aliyepachika bao la kwanza kwenye ligi huku Morrison yeye akitoa pasi ya bao kwa Bakari Mwamnyeto ilikuwa dk ya 84.

Aziz ki
Morisson

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga alisema kuwa anafurahi kuona kila mchezaji anatimiza majukumu yake jambo ambalo linawapa matokeo.


Kwa Taarifa za Kimichezo na Habari za Uchambuzi Unaweza Kutazama Video zetu Kupitia youtube  Meridianbet Tanzania

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa