BAADA ya kuwatambulisha nyota wao watano, Uongozi wa Dodoma Jiji umeweka mikakati ya kumaliza ligi katika nafasi tano za juu kwenye msimamo wa ligi.

Nyota hao waliosajiliwa mpaka sasa ni Collins Opare, Christian Nziga, Randy Bangala, Paul Peter, na Aman Kiyata.

Akizungumzia hilo, Mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Dodoma Jiji, Fredrick Mwakisambwe alisema kuwa “Tumefanikiwa kunasa saini za wachezaji ambao wataongeza nguvu kwenye kikosi chetu na watano tumewatangaza tayari.

“Malengo yetu tuliyojiwekea kwa msimu ujao ni kumaliza kwenye nafasi tano za juu na katika kutimiza hayo tunatarajia kuanza kambi yetu Julai 15 mwaka huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa