Uongozi wa klabu ya Simba umeweka wazi kukamilisha sajili zao zote za msimu huu huku wakiweka wazi kilichobaki kwa sasa ni kusubiri utambulisho tu wa wachezaji wao akiwemo mshambuliaji mwenye uraia wa Nigeria Nelson Okwa.

Simba tayari imeshatambulisha majembe yake kama Moses Phiri,Nasoro Kapama,Habib Kyombo,Victor Akpan huku wakitarajiwa kuwatambulisha wachezaji wengine kama Nelson Okwa,Augustine Okrah na beki Mohammed Outtara.

Habari za ndani kabisa zinasema Nelson Okwa na Mohammed Outtara ndio watafunga usajili ndani ya Simba kwa msimu huu mara baada ya sajili nyingine kukamilika jambo ambalo litawafanya kuwatambulisha mwishoni wachezaji hao.

Chanzo cha habari hiyo kilifunguka kuwa: “Simba imekamilisha tayari sajili zake zote na kilichobaki ni kuwatambulisha tu na kuna baadhi ya wachezaji waliku wa mwisho kama Okwa na Outtara katika kukailisha mazungumzo yao na wanaweza kuwa wa mwisho kwenye utambulisho wao.”

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmedy Ally akizungumza na waandishi wa habari jana alisema:”Kwa sasa kila kitu kipo kamili na tumeshakamilisha sajili za wachezaji wetu wote ambao tuliwahitaji na kilichobaki kwa sasa ni kuhakikisha kuwa tunakamilisha taratibu za kuwatambulisha wachezaji hao.”

“Na usajili huu tayari tulishamtumia majina Kocha wetu mpya wa Simba mpya na tayari amewafuatilia wachezaji hao huku nay eye akiongeza jina la mchezaji mmoja ambaye tayari pia tumeshamalizana naye.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa