BAADA ya kufanikiwa kubaki kwenye michuano ya ligi kuu kwa msimu ujao, Uongozi wa Mtibwa Sugar umefunguka kufanya maamuzi magumu katika kikosi chao kwa msimu ujao.

Mtibwa walipata nafasi ya kubaki ligi kuu baada ya kuiondosha Tanzania Prisons katika mchezo wa mtoano.

Akizungumzia usajili wao, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa “Tunaendelea na vikao kwa ajili ya kujadili ni kwanini timu yetu kwa misimu miwili ilicheza playoff.

“Katika usajili tunatarajia kufanya maamuzi magumu ili kuhakikisha tunaboresha zaidi kikosi chetu lakini baada ya hivi vikao tutatoa idadi ya wachezaji ambao tutawaacha na wale wanaoingia kwenye timu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa