WAKATI Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Kim Poulsen akitangaza wachezaji 25 watakaoingia kambini Agosti 21, mwaka huu, nyota wawili wameongezwa kwenye kikosi hicho ambao ni Beno Kakolanya na Habib Kyombo.

Nyota hao wataingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili dhidi ya Uganda kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za CHAN.

stars, Kakolanya na Kyombo Kuongeza Mzuka Stars, Meridianbet

Nyota wengine ni Aishi Manula, Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Shomary Kapombe, Mohamed Hussein, Pascal Msindo, Nathan Chilambo, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto.

Kenedy Juma, Sospeter Bajana, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Kelvin Nashon, Feisal Salum, Salum Aboubakar, Farid Mussa, Abdul Selemani, Relliants Lusajo, Kibu Denis, George Mpole, Anuary Jabir, na Danny Lyanga.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa