Harry Maguire nahodha wa klabu ya Manchester United  ataukosa mcheo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Manchester City dhidi Manchester United utakaopigwa siku ya jumapili.

harry maguireBeki huyo alieitumikia timu ya taifa ya Uingereza katika michezo ya Uefa Nations League ambapo timu hiyo imeshuka daraja katika michuano hiyo beki huyo ndipo alipopata majeraha akiitumikia timu yake ya taifa na kusababisha kuukosa mchezo dhidi ya mahasimu wa katika jiji la Manchester.

Harry Maguire ambaye siku za hivi karibuni amekua akipokea shutuma kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kushuka uwezo kwa kiwango kikubwa katika mechi alizotumikia timu hiyo pamoja na timu ya taifa amekua hana kiwango cha kuridhisha.

harry maguireHarry Maguire amekua akieleza kuhusu kiwango chake na kusema watu wa vyombo vya habari wanamuandika kwasababu yeye ni nahodha wa Man United na wakimuandika wanajua habari zao zitauza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa