Dirisha La Usajili Limefunguliwa Leo

Dirisha dogo la usajili kwa klabu za ligi kuu, ligi daraja la kwanza, na ligi kwa wanawake limefunguliwa rasmi hii leo Desemba 16, 2022 na litafungwa Januari 15 2023.

 

Dirisha La Usajili Limefunguliwa Leo

Shirikisho hilo limesisitiza kuwa vilabu vinatakiwa kutumia muda huo uliowekwa kwaajili ya kufanya usajili ili waweze kununua na kuuza wachezaji ambao wanaowataka kabla ya dirisha kufungwa.

Dirisha hili ni kwaajili ya timu ambazo zinaona zina uhitaji wa wachezaji kwenye klabu yao na pia kama wakikutana na changamoto yoyote wakati wa usajili iwasiliane na idara ya mawasiliano TFF.

Dirisha La Usajili Limefunguliwa Leo

TFF pia imesisitiza kuwa baada ya dirisha hili kufungwa hakutakuwa na muda wa ziada, hivyo ni vyema vilabu vikakamilisha usajili na uhamisho kwa wakati.

Kuna vilabu ambavyo tetesi kwa upande wao zimeanza kuvuma kuwa zinamhitaji mchezaji huyu na huyu hivyo mpaka kufikia mwisho vitakuwa vimekamilisha.

Acha ujumbe