Gwiji wa zamani wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard ana matumaini makubwa ya klabu yake hiyo ya zamani kufanya vizuri baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika.

Klabu ya Liverpool ambayo ilkua na msimu bora sana mwaka 2021/22 ambapo walikua kwenye nafasi kubwa ya kutwaa mataji manne, Lakini wakaambuliwa mataji mawili ambapo hali imekua tofauti kidogo na msimu huu.gerrardKlabu ya Liverpool imekua kwenye wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu huu ambapo klabu hiyo imekua ikipoteza alama mara kwa mara, Kitu kilichofanya klabu hiyo kushika nafasi ya sita kwenye ligi kuu ya Uingereza na kukaa nyuma kwa alama 15 nyuma ya vinara klabu ya Arsenal.

Nahodha wa zamani wa klabu hiyo Gerrard anaamini klabu hiyo itarudi na nguvu kwenye miezi sita hii ya kumalizia msimu, Liverpool haijakua na msimu mzuri kabisa kitu ambacho gwiji huyo anaamini timu hiyo itakibadilisha kwenye ungwe ya mwisho ya kumalizia msimu.gerrardGwiji Gerrard anaamini mapumziko haya kupisha michuano ya kombe la dunia yameipa ahueni klabu yake hiyo ya zamani kuweza kujipanga vema na kurejesha makali yao, Nahodha huyo wa zamani wa klabu hiyo anaamini kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp na benchi lake la ufundi watarudi imara zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa