KLABU ya KMC unaweza kusema wameamka kwenye usingizi mzito wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa tayari mzunguko wa pili umeanza kwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Wagosi wa kaya Coastal Union ya Tanga.

Pamoja na urejeo wa nyota wao Awesu Awesu, Steve Nzigamasabo na Matheo Anthony ambao walizikosa mechi kadhaa nyuma ikiwemo ile ya Tanzania Prisons, KMC walicheza soka zuri ambalo liliwafanya kuwalaza na viatu Wagosi wa kaya na kulipa kisasi cha mzunguko wa kwanza ambao walipoteza wakiwa mkoani Arusha.

Kocha wa KMC Thiery Hitimana alisema kuwa timu yake imecheza vizuri lakini wanapaswa kurekebisha baadhi ya maeneo.kmc“Tumecheza vizuri, niwapongeze wachezaji wangu lakini tunapaswa kurekebisha na kuboresha baadhi ya maeneo kwenye dirisha hili dogo”

Matukio Yaliyotokea kwenye Mchezo.
Matheo Anthony Kuumia.
Unaweza kusema moja ya sababu ya KMC kutopata matokeo mazuri ni pigo la kumkosa mshambuliaji wao namba 1 Matheo Anthony aliyeumia kwenye kipindi cha kwanza, hali iliyopelekea kutolewa nje kwa matibabu zaidi.

Uzembe wa kutotumia nafasi za wazi

Timu zote mbili walikosa umakini kwenye eneo la mwisho haswa katika kuzitumia nafasi za magoli kuwa goli, KMC walitengeneza nafasi zaidi ya mbili lakini walishindwa kupata bao, nao Coastal Union waliweza kutengeneza nafasi nyingi kiwazidi KMC ila unaweza kusema ubunifu kwenye eneo la umaliziaji ulikosekana.kmcBaada ya mchezo huu KMC watakutana na Polisi Tanzania wiki ijayo kabla ya kukutana na Simba SC mkoani Mwanza Disemba 26, 2022.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa