Fernando Santos: Aondoka Timu ya Taifa ya Ureno

Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos ameachana na timu hiyo leo baada ya kuondolewa kwenye michuano ya kombe la dunia kwenye hatua ya robo fainali.

Kocha huyo  ambaye amefanikiwa na timu ya taifa ya Ureno na kufanikiwa na kuipa taji la kwanza taifa hilo la kwanza la michuano ya Euro 2016, na taji Uefa Nations League mwaka 2019 na kuingia kwenye vitabu va historia vya nchi hiyo.fernando santosKocha Fernando Santos anaondoka timu ya taifa ya Ureno baada ya kudumu kwa muda mrefu kwenye timu hiyo na kupata mafanikio makubwa, Taarifa zinaeleza kocha huyo hajafukuzwa kwenye timu hiyo na alipanga tangu awali akimaliza michuano ya kombe la dunia anaachana na timu hiyo.

Shirikisho la soka nchini Ureno inaelezwa wanatarajia kumtangaza mrithi wa Fernando Santos wiki kadhaa zijazo, Taarifa za ndani zinaeleza shirikisho hilo linatafuta kocha mwenye uwezo mkubwa wa kuweza kuongoza kizazi hichi cha Ureno ambacho kinaonekana ni kizazi cha dhahabu.fernando santosTaarifa za ndani zinaeleza kua shirikisho la soka nchini Ureno linapanga kumpa timu kocha mreno mwenye mafanikio makubwa kwenye ulimwengu wa soka Jose Mourinho, Huku wakitaka kumruhusu aendelee kufundisha pia klabu yake ya As Roma.

Acha ujumbe