Glazer: Mchakato wa Kuiuza United Unaendelea

Mabosi wa klabu ya Manchester United wanaojulikana kama Glazer Family wamesema mchakato wa kuiuza klabu hiyo bado inaendelea ambayo ilitangazwa kuuzwa wiki kadhaa nyuma.

Klabu ya Manchester United imewekwa sokoni tangu mwezi uliopita na wamiliki hao wa klabu hiyo ambao wanaimiliki klabu hiyo toka mwaka 2005, Na siku za hivi karibuni wameonekana wakipata pingamizi sana kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo mpaka kufikia uamuzi wa kuiza timu hiyo.glazerMiongoni mwa wamiliki wa klabu hiyo ambaye anajulikana kama Avram Glazer alikuepo katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Morocco katika dimba la Al Bayt, Huku akiulizwa na waandishi kuhusu mchakato wa kuiuza klabu hiyo unaendeleaje na kueleza kua bado wanaendelea na mchakato huo na watu wasubiri kuona nini kitatokea.

Manchester United na familia ya Glazer wamekua kwenye ndoa ya muda mrefu kwa takribani miaka 17 sasa tangu 2005 huku wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo, Lakini kwasasa mashabiki wa klabu hiyo wanahitaji mabadiliko ndani ya timu hiyo na kuhitaji familia hiyo iachie timu.glazerKlabu hiyo pendwa kabisa nchini Uingereza ka miaka ya hivi karibuni imeonekana kupoteza ule ubora wake kwa kiwango kikubwa kitu ambacho kimewafanya mashabiki wa timu hiyo kuona ni muda sahihi wa wamiliki hao kuachia ngazi kutokana na muenendo wa klabu yao.

Acha ujumbe