Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo mzunguko wa pili, mechi ya 16 ambapo timu ya KMC watakuwa uwanjani kuwaalika Coastal Union ya mkoani Tanga majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Uhuru.

 

KMC Kumualika Coastal Union Uhuru Leo

KMC wapo nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 15 hadi sasa, ushindi mara tatu, sare saba na kupoteza mara tano wakijikusanyia pointi zao 16. Lakini hawajapata ushindi mechi saba mfululizo.

Wakati Wagosi wa Kaya wao wapo nafasi ya 12, michezo 15 wamecheza, ushindi mara nne, droo tatu, na kupoteza michezo nane, wakiwa na pointi zao 15 kibindoni. Coastal wao wakiwa wametoka kushinda mechi yao iliyopita.

KMC Kumualika Coastal Union Uhuru Leo

Mechi ya mwisho kukutana Coastal Union walishinda na kujiondokea na pointi tatu muhimu, huku mechi ya leo KMC ya Hitimana ikiangaliwa itafanya nini baada ya kutopata matokeo muda mrefu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa