Rais wa Ufaransa Emanuel Macron amemsifu kiungo wa timu ya taifa ya Morocco Sofyan Amrabat na kumuambia kama kiungo bora wa mashindano ya kombe la dunia mwaka huu.

Kiungo huyo amekua na kiwango bora sana kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na kuisaidia timu ya taifa ya Morocco kufika nusu fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia ya soka la Afrika.sofyan amrabatKiungo Sofyan Amrabat ambaye anakipiga katika klabu ya soka ya Fiorentina ya nchini Italia amekua akizungumzwa zaidi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco, Na hii ni kutokana na kua mchezaji muhimu na nguzo kwenye kikosi hicho chini ya kocha Walid Regragui.

Rais wa Ufaransa inaelezwa usiku wa jana baada ya Ufaransa kuifunga Morocco katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia kwa mabao mawili kwa bila alikwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya Morocco na kumuambia kiungo huyo amekua kiungo bora wa mashindano mbele yawachezaji wenzake.sofyan amrabatKiungo Sofyan Amrabat amekua kwenye ubora mkubwa kwenye kombe la dunia na kufanya vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya kuanza kumnyatia kiungo huyo fundi mzaliwa wa Uholanzi kutokana na ubora wake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa