Ishu ya Bangala na Djuma Kutoka Yanga Ipo Hivi

Djuma Shaban na Yannic Bangala wanatajwa kuomba kuondoka ndani ya kikosi cha Yanga.

 

Ishu ya Bangala na Djuma Kutoka Yanga Ipo Hivi

Habari zinaeleza kuwa kuondoka kwa Nasreddine Nabi ndani ya Yanga kwenye benchi la ufundi kunawafanya mastaa wengine kufikiria kuondoka pia.

Ipo wazi kuwa Bangala mkataba wake bado unaishi ndani ya Yanga kama ilivyo kwa Djuma mpaka 2024 lakini wanahitaji kuondoka.

Djuma ameomba kuondoka Yanga ili kupata changamoto mpya na Bangala pia ameomba kusepa licha ya kuwa na mkataba wa mwaka mmoja.

Ishu ya Bangala na Djuma Kutoka Yanga Ipo Hivi
Hivi karibuni ilielezwa kuwa Bangala ana asilimia 20 za kubaki ndani ya Yanga kwa msimu ujao wa 2023/24.

Kuhusu mikataba ya wachezaji Injinia Hersi Said aliweka wazi kuwa watafanya maboresho makubwa kwa ajili ya timu hiyo na kuwaboreshea mikataba wachezaji

Acha ujumbe