Bacca Kuvuna Mkwanja Mrefu Yanga

Beki wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 Ibrahim Hamad Bacca ataboreshewa mshahara pamoja na mkataba wake.

 

Bacca Kuvuna Mkwanja Mrefu Yanga

Beki huyo bado yupo ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kusaini dili la miaka mitatu ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.
Ni mwepesi kwenye kuzuia hatari ndani ya 18 na nje ya 18 kwenye mipira ya juu pia ameonyesha uimara kwa kuokoa hatari za mapigo ya kona na mipira ya kurusha.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa kwa wachezaji waliofanya vizuri kuna maboresho juu yao na wataendelea kuboresha kila wakati.

“Tunafanya maboresho kwa wachezaji wetu ikiwa ni pamoja na Bacca tunaamini amefanya kazi nzuri na bado ana mkataba na Yanga hivyo bado yupo.”

Bacca Kuvuna Mkwanja Mrefu Yanga

Kikubwa ni kuwa kwenye mwendelezo bora na ambacho tunakifanya kwa wachezaji wote ni kuzungumza nao ili waendelee kufurahia kutimiza majukumu yao ndani ya Yanga.

Bacca alikuwa kwenye kikosi kilichoshuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukisoma Azam FC 0-1 Yanga katika fainali ya Azam Sports Federation.

Yanga pia ni mabingwa wa taji hilo ambalo walilitwaa pia msimu wa 2021/22.

Acha ujumbe