Manchester United Yavutiwa na Dimarco

Klabu ya Manchester United inavutiwa na beki wa kushoto wa klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Federico Dimarco kwajili ya kuboresha kikosi chake kwajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Uingereza.

Manchester United inamuhitaji Dimarco kwajili ya kuboresha eneo lake la ulinzi ambalo halina mbadala sahihi pale anapokosekana beki wa kimataifa wa Uingereza Luke Shaw, Hivo Dimarco amneonekana kama mtu sahihi wa kucheza upande huo wa kushoto.Manchester UnitedFederico Dimarco amekua na msimu mzuri sana ndani ya kikosi cha Inter Milan ambacho kimefanikiwa kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu huu, Lakini pia beki huyo wa kimataifa wa Italia amekua sehemu ya mafanikio ya kikosi hicho.

Manchester United inatarajia kukutana na upinzani mkubwa katika nafasi hiyo kwani mchezaji huyo anawindwa pia na wababe wa soka kutoka nchini Hispania klabu ya soka ya Real Madrid ambao nao wameonesha uhitaji kwa beki huyo.Manchester UnitedKlabu ya Manchester United haijafanya usajili wowote mpaka sasa hivi kwenye dirisha hili kubwa majira ya haya joto hivo wanahitaji kuboesha kikosi chao kuelekea msimu ujao na beki Dimarco anaonekana kama mtu sahihi wa kuanza nae kwenye dirisha hili.

Acha ujumbe