Klabu ya Kagera Sugar ambayo inaongozwa na kocha mkuu Mecky Mexime imeibuka na pointi tatu muhimu katika mchezo wao wa 14 wa Sugar Derby dhidi ya Mtibwa ambao umepigwa hii leo majira ya saa 8:00 mchana CCM Kirumba.
Bao hilo la Kagera Sugar limefungwa kipindi cha pili cha mchezo dakika ya 67 na Abraham Mwamita baada ya kwenda mapumziko bila kufungana na ndipo kipindi cha pili kikabadilisha ubao wa matokeo kwa upande wa Wanankurukumbi.
Licha ya matokeo hayo Kagera wanaendelea kusalia katika nafasi yao ya 9 na kujiongezea pointi 18 kwenye ligi mpaka sasa huku Mtibwa nao wakisalia kwenye nafasi yao ya 6 baada ya kupoteza mchezo wa leo.

Baada ya kupoteza mchezo wao leo timu ya Mtibwa itasafiri hadi Geita kukipiga dhidi ya wachimba madini Geita Gold, huku Mexime yeye atamualika Ihefu nyumbani kwake kutafuta alama tatu zingine.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA



