Kipa wa Inter Milan na timu ya Taifa ya Cameroon Andre Onana ameondolewa kwenye kikosi cha Cameroon ambacho hii leo kimecheza dhidi ya Serbia kutokana na sababu za kinidhamu.

Onana ambaye ana miaka 26 anachukua mikoba kutoka kwa Samir Handanovic huko Inter Milan na inaonekana kuwa chaguo lao la muda mrefu katika klabu hiyo ambayo inaongozwa na Simone Inzaghi.
Onana alisajiliwa na Inter kwa uhamisho huru msimu wa joto baada ya muda wake na Ajax kumalizika na akajumuishwa kwenye kikosi taratibu, na kusalia kwenye benchi kwa mechi nane za kwanza za Serie A msimu huu.

Kama ilivyoripotiwa na RMC Sport, Onana alicheza dakika zote 90 za mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia la Cameroon dhidi ya Uswizi lakini hatacheza michezo ijayo huko Qatar kwa sababu za kinidhamu.
lKipa Devis Epassy amechukua nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza na Onana hata hajakaa benchi kwenye pambano la Serbia huku baadhi ya taarifa zikisema ameondolewa moja kwa moja.

Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


