United Wanakaribia Kumnasa Nyota wa Uholanzi Gakpo

Klabu ya Manchester United ambayo ipo chini ya kocha mkuu Eric Ten Hag wanakaribia kuinasa saini ya nyota wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo mwenye umri wa miaka 23.

 

United Wanakaribia Kumnasa Nyota wa Uholanzi Gakpo

Gakpo, amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu na amepeleka huo ubora wake kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa kuanza kupachika mabao kwenye Eredivisie na  kwenye Kombe la Dunia.

Akiwa ameifungia Uholanzi mara mbili katika mechi zao mbili za mwanzo, atatumaini kuwa mchezaji wa kutegemewa kwa mara nyingine hapo kesho huku vijana wa Louis van Gaal wakipania kutinga hatua ya 16 bora dhidi ya Qatar.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uholanzi, Gakpo amejulikana kama mchezjibambayo yupo kwenye rada wa za united na Erik ten Hag amependekeza kuwa waajiri wake wamsajili mchezaji huyo.

United Wanakaribia Kumnasa Nyota wa Uholanzi Gakpo

Mshambuliaji huyo mahiri amefunga mabao tisa na kupiga asisti 12 katika mechi 14 za ligi akiwa na PSV hadi sasa msimu huu, huku ESPN ikiripoti kwamba Raphael Leao na Christian Pulisic pia wako kwenye mbio za United na wote waking’aa kwenye timu zao za Kitaifa Kombe la Dunia.

Uhamisho wowote wa nyota wa Marekani Pulisic, 24, unaweza kuwa mkataba wa mkopo kwa vile Chelsea haitakuwa na nia ya kumuuzia mpinzani wake wa moja kwa moja, huku nyota wa Ureno Leao, 23, angegharimu ada kubwa kutokana na uwezo wake mkubwa na hali ya kandarasi katika klabu ya AC Milan.

United Wanakaribia Kumnasa Nyota wa Uholanzi Gakpo

Kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ndio kipaumbele cha Ten Hag, ambaye bado hajaridhishwa na kikosi chake cha kwanza cha United licha ya kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

odds kubwa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.