Kocha mkuu wa Hispania Luis Enrique amewafaraji wachezaji wake kwa kutoa sare ya jana na kuridhika na ukweli kwamba timu yao inaelekea mechi ya mwisho ya Kundi E ya Kombe la Dunia kama viongozi.

Bao la Alvaro Morata kipindi cha pili lilionekana kuwaweka Hispania kwenye mkondo wa ushindi wa pili katika mechi nyingi za kundi, na ushindi ungeihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora, lakini Niclas Fullkrug akasawazisha bao hilo kwa Ujerumani na kufanya wagawane pointi moja moja.
Licha ya kutoa sare hiyo ukweli ni kwamba Hispania inasalia katika nafasi ya kwanza ya kundi hilo ikiwa na pointi nne katika kundi hilo ingawa wanaweza kuwa katika hali nzuri zaidi ambapo watapata ushindi mechi yao ya mwisho.
Enrique amesema kuwa; “Kinadharia hili lilikuwa kundi la kifo, na kama baada ya sare tungeambiwa kwamba baada ya mechi mbili za kwanza tutakuwa viongozi wa kundi na tunajitegemea sisi wenyewe, wachezaji wametia saini kwa hilo.”

Enrique amewaambia waandishi wa habari kuwa sare dhidi ya Japan inatosha lakini hawatakisia, lakini inabidi wafurahi kwasababu wao ni viongozi wa kundi hilo la kifo., huku kila mmoja alishangazwa na sre ya jana kwani lilikuwa kundi la kuvuta hisia.
Kocha wa Hispania Luis Enrique alihisi Ujerumani walikuwa wanastahili kupata pointi, ingawa pia aliona timu yake ikipoteza nafasi ya kuwamaliza kabla ya Fullkrug kusawazisha.
“Ujerumani ni nguvu ya mpira wa miguu. Hatuwezi kuwatenga kwa kushinda Kombe la Dunia, lakini tulipambana.”

Hispania itamenyana na Japan siku ya Alhamisi ikijua ushindi utawafanya wapate pointi 6 na kukaa kileleni huku Ujerumani ikizichapa dhidi ya Costa Rica wakati huo huo wakitumai kupanda kutoka mkiani hadi kufuzu.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


