Onana Apata Ajari ya Gari Wakati Akielekea Kambini

Golikipa wa Ajax Andre Onana amepata ajali mbaya ya gari wakati akielekea kuungana na timu ya taifa ya Cameroon siku ya leo.

Onana Apata Ajari ya Gari Wakati Akielekea Kambini

Onana alikuwa anasafiri kutoka jijini Yaounde mpaka Douala ambako timu ya Cameroon wameweka maskani yao kwaajili ya mchezo wa mtoano wa Kombe la Dunia dhidi ya Algeria.

Vyombo vya habari vya ndani vilionyesha picha za gari alilokuwa akisafiria Onana, na gari lingine, huku sehemu ya mbele ya kila moja ikiwa imeharibika vibaya.

Onana, 25, alichukuliwa kutoka eneo la ajali hadi kituo cha timu ya Cameroon na kupigwa picha, akionekana kutojeruhiwa; hata hivyo, iliamuliwa aende kuchunguzwa hospitali.

“Andre Onana yuko sawa,” ukurasa rasmi wa Twitter wa timu hiyo ulisema. “Kipa huyo wa Indomitable Lions alijiunga na wachezaji wenzake kwenye kambi huko Douala asubuhi ya leo.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe