Kocha mkuu wa timu ya taifa Uholanzi Louis van Gaal amekutwa na maambukizi ya coronavirus kuelekea mechi za kirafiki dhidi ya Denrmark na Ujerumani na nafasi yake itachukuliwa na Danny Blind, Henk Fraser na Frans Cruijff.
Uholanzi wanatarajiwa kuumana na Ujerumani siku ya Jumamosi huko Amsterdam ambapo bosi huyo hatokuwepo akiwa anaendelea kujitenga kama taratibu zinavyotaka pindi mtu anapopatwa na maambukizi.
Netherland tayari wamefuzu kucheza kombe la Dunia huko Qatar 2022 baada ya kuifunga Norway kwa 2-0 mwezi Novemba na wakiongoza kundi G.
Uholanzi, wamefuzu mara tatu kufika fainali ya Kombe la Dunia, alishindwa kufuzu fainali za michuano hiyo nchini Urusi. Van Gaal hapo awali aliifundisha Uholanzi hadi nusu fainali kwenye Kombe la Dunia la 2014 huko Brazil.
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.