KIONGOZI SIMBA: "AL AHLY TULIKUWA TUNAWATAKA"

Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba ameibuka na kutamba kuwa Al Ahly ya nchini Misri waliokuwa wanataka kupangwa nao ndiyo timu au wapinzani ambao walikuwa wanaomba kukutana nao.

 

KIONGOZI SIMBA: "AL AHLY TULIKUWA TUNAWATAKA"

Timu hizo zitakutana katika michuano ya Caf African Football League Oktoba, mwaka huu kwenye mchezo wa ufunguzi utaochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba tayari imeanza maandalizi ya michuano hiyo, pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuingia kambini wiki iliyopita .

Ahmed alisema kuwa wanajivunia uzoefu wao wa kucheza michuano mikubwa, hivyo ana matumaini ya timu hiyo, kufanya vema.

KIONGOZI SIMBA: "AL AHLY TULIKUWA TUNAWATAKA"

Ahmed alisema kuwa anaheshimu ukubwa wa Al Al Ahly, lakini hiyo haiwafanyi iwaogope kutokana na usajili bora ambao wameufanya msimu huu.

Aliongeza kuwa wachezaji wao wameonekana kufurahi kupangiwa na Al-Ahly wakionyesha kuuhitaji mchezo huo.

Al Ahly tunawaheshimu, lakini hatuwaogopi, kwani ni kati ya klabu kubwa Afrika, hivyo hatuwahofii tutakapokutana nao. Kikubwa tunakwenda katika mchezo huo tukiwa tukihitaji ushindi na sio kitu kingine tutakapokutana.

KIONGOZI SIMBA: "AL AHLY TULIKUWA TUNAWATAKA"

“Kama ilivyokuwa kawaida yetu katika michuano ya kimataifa, hatutakubali kupoteza mchezo wowote wa nyumbani,” alisema Ahmed.

Acha ujumbe