Simba Kumenyana na Al Ahly

Klabu ya Simba itakutana uso kwa uso na mabingwa wa Afrika klabu ya Al Ahly katika michuano ya African Football League baada ya droo kuchezeshwa leo.

Simba ambayo ni timu pekee kutoka Tanzania kushiriki michuano hiyo ambayo ni mipya na yenye thamani zaidi kwasasa wamepangwa na Al Ahly katika mchezo wao wa kwanza ambao utapigwa katika mikondo miwili.simbaWekundu wa Msimbazi wanapaswa kuhakikisha wanapata matokeo katika michezo miwili ambayo watamenyana na klabu ya Al Ahly kwani kama watafanikiwa kupata matokeo mazuri watakwenda hatua ya nusu fainali moja kwa moja.

Michuano ya African Footbal League imeshirikisha timu nane tu ambazo zina ubora kutoka barani Afrika,Hivo kwenye michezo hii ya awali timu nne ndio zitaweza kusonga mbele kama zitapata matokeo na zingine nne zitafungasha virago.simbaKlabu ya Simba na Al Ahly kwenye miaka ya karibuni wamekutana mara nne huku Mnyama akiokota alama sita kwa maana ya kushinda michezo miwili kama ambavyo imekua kwa Al Ahly, Hivo inaonesha ni timu ambazo zinaweza kupambana na yeyote anaweza kufuzu hatua ya nusu fainali.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.