Bellingham Aendelea Kuibeba Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uingereza Jude Bellingham ameendelea kua mwokozi wa klabu ya Real Madrid baada ya kufunga tena leo.

Bellingham amefanikiwa kufunga bao la ushindi katika mchezo wa Real Madrid ambao walikua nyumbani dhidi ya klabu ya Getafe, Bao alililofunga kiungo huyo ndio ambalo limepeleka alama tatu moja kwa moja kwa Real Madrid.bellinghamKlabu ya Real Madrid ilikua imeshatanguliwa kwa bao moja na klabu ya Getafe mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko, Lakini kipindi cha pili Madrid walirudi kwa kasi na kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji Joselu.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingerereza alifunga bao la ushindi katika dakika za nyongeza akiendelea ambapo ameishia katika michezo iliyopita ya klabu hiyo kwani ndio amekua mchezaji bora wa timu hiyo mpaka sasa.bellinghamKiungo Jude Bellingham ambaye ametoka kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Hispania kwa mwezi wa nane mpaka sasa amefanikiwa kuhusika kwenye mabao sita ndani ya timu katika michezo minne aliyocheza mpaka akifanikiwa kufunga mabao matano na kupiga pasi moja ya bao.

Acha ujumbe