Heung Ming Son Amewaka Spurs

Nahodha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Heung Ming Son ameanza kuwasha moto ndani ya klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London kutokana na kiwango alichokionesha leo.

Tottenham leo wameibamiza klabu ya Burnley kwa mabao matano kwa moja na Heung Ming Son akiwa kwenye kiwango bora kabisa katika mchezo huo ambapo alifanikiwa kufunga mabao matatu.heung ming sonNahodha huyo wa klabu ya Tottenham alionekana kama ameanza vibaya msimu huu  lakini sasa ni wazi ameanza kurejesha makali yake ambayo yameonekana katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Burnley chini ya kocha Vicent Kompany.

Winga huyo ambaye amekua kwenye ubora miaka mingi ndani ya klabu ya Tottenham baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa leo amefanikiwa kufikisha mabao 104 katika ligi kuu ya Uingereza na kuwapita nyota mbalimbali kama Cristiano Ronaldo, na Didier Drogba.heung ming sonHeung Ming Son baada ya kufanikiwa mabao matatu kwa bila katika mchezo wa leo na kuiwezesha klabu yake kupata ushindi mnono wa mabao matatu, Lakini pia klabu ya Tottenham inaendelea kua moja ya timu ambazo hazijapoteza mchezo wakiwa na alama zao 10 nafasi ya pili kwenye msimamo.

Acha ujumbe