Heung Ming Son Nahodha mpya Spurs

Winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs raia wa kimataifa wa Korea Kusini Heung Ming Son amefanikiwa kutangazwa kama nahodha mpya wa klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London.heung ming sonWinga huyo ametangazwa kua nahodha klabuni hapo baada ya aliyekua nahodha wa klabu hiyo golikipa Hugo Lloris kutimka klabuni hapo, Lakini pia aliyekua nahodha msaidizi ambaye alitarajiwa kua nahodha mkuu msimu huu Harry Kane na yeye kutimkia klabu ya Fc Bayern Munich.

Winga Heung Ming Son wakati akizungumzia tukio hilo la kupewa unahodha alisema “Ni heshima kubwa kwangu kua nahodha kwa klabu hii, imekua suprise kubwa kwangu lakini pia tukio la kujivunia sana, Nimewaambia wachezaji wenzangu kila mmoja anapaswa kujihisi na nahodha ndani na nje ya kiwanja”heung ming sonHeung Ming Son amekua moja ya wachezaji muhimu wa klabu ya Tottenham Hotspurs tangu alipojiunga klabuni hapo mwaka 2015 klabuni hapo akitokea klabu ya Bayern Leverkusen ya nchini Ujerumani.

Winga huyo baada ya kutangazwa kua nahodha wa klabu ya Tottenham ni wazi kwasasa anakua nahodha wa timu mbili, Kwani mchezaji huyo pia ni nahodha wa timu yake ya taifa ya Korea Kusini.

 

Acha ujumbe