Winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza Heung Ming Son amefanikiw kushinda tuzo ya mchezaji bora wa bara la Asia kwa mara ya sita mfululizo.
Heung Ming Son amekua akifanya vizuri ndani ya klabu ya Tottenham kwa misimu kadhaa na kumfanya kushinda tuzo ya mchezaji bora kutoka bara Asia, Mchezaji huyo ametangazwa kama mchezaji bora barani humu na kumfanya kubeba tuzo hiyo kwa mwaka wa sita mfululizo.
Baada ya kubeba tuzo hiyo Heung Ming Son anakua amekamilisha tuzo nane kama mchezaji bora wa bara la Asia kwa miaka tofauti tofauti. Huku hii ya mara sita mfululizo ikiwa ni rekodi nzuri zaidi kwa upande wake akifanya hivo kuanzia mwaka 2018 mpaka mwaka 2023.
Winga huyo anayechezea klabu ya Tottenham pamoja na timu ya taifa ya Korea Kusini amefanikiwa kubeba tuzo hiyo ikiwa sio mafanikio na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu yake, Lakini pia amekua na mchango mkubwa sana katika timu yake ya taifa ya Korea Kusini.
Mchezaji huyo ambaye alianza kufanya vizuri katika ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga katika vilabu vya Hambuger Sv pamoja na Bayern Leverkusen kabla ya kuhamia ligi kuu ya Uingereza amefanikiwa kushinda tuzo hiyo kwa mara nane mpaka sasa.

