Mshambuliaji wa Namungo FC Reliants Lusajo ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi kuu ya NBC mpaka sasa baada ya kufunga mabao 06 katika michezo 10 ambayo timu yake wamekwishacheza.

 

Lusajo Kinara wa Mabao Mpaka Sasa

Baada ya Lusajo, anayefuata kwa mabao mengi ni Mosses Phiri wa Simba mwenye mabao matano, na Sixtus Sabilo wa Mbeya City nae pia ana mabao matano kwenye Ligi kuu ya Tanzania Bara.

Lusajo na timu yake wapo nafasi ya sita baada ya kushinda michezo minne, wameenda sare mara tatu na wamepoteza michezo mitatu tu mpaka sasa na wamejikusanyia pointi 15 tu.

Namungo ambaye amepanda Ligi msimu juzi na kumaliza nafasi ya nne ambayo ilimfanya ashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na kutolewa katika hatua za mtoano ameanza vyema msimu huu.

Lusajo Kinara wa Mabao Mpaka Sasa

Mechi inayofuata watakipiga dhidi ya Simba Tarehe 16 huku toka wakutane kwenye Ligi Namungo hajawahi kushinda mchezo wowote zaidi ya kupata sare na vipigo.


AVIATOR

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa