Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Fiston Kalala Mayele amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi kuu ya NBC Primia Ligi msimu huu kufunga Hat-trick tangu msimu huu wa 2022/2023 uanze.

 

Mayele Apiga Hat-trick ya Kwanza NBC Primia Ligi

Mayele alitupia mabao hayo kwenye mchezo wa jana walipokuwa wakicheza dhidi ya Singida Big Stars na kufanikiwa kuwafunga kwa mabao 4-1 na Young Africans kuondoka na pointi 3 muhimu.

Mabao hayo ya Fiston aliyafunga katika dakika ya 16, 27, 56 na baadae katika kipindi cha pili dakika ya 48 beki wa pembeni Kibwana Shomari akatupia bao la nne katika dakika ya 48 na kufanya Walima alizeti wawe na mlima mkubwa wa kupanda.

Singida walionekana jana kuzidiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ubora ambao Yanga waliouonyesha kuanzia mbele hadi nyuma huku Fiston akielekeza ushindi huo wa mabao hayo kwa mtoto wake aliyempata na mke wake.

 

Mayele Apiga Hat-trick ya Kwanza NBC Primia Ligi

Dakika ya 66 ya mchezo mshambuliaji wa Singida Medie Kagere anaifungia timu hiyo ya Pluijim lakini bao hilo halikutosha hata wao kuambulia sare kwenye mchezo huo kwani wapinzani wao walikaa imara.

Ushindi huo wa Yanga umewafanya wapae kileleni kwenye msimamo wa Ligi baada ya kufikisha pointi zao 26 sawa na Azam japokuwa Nabi bado ana michezo miwili mkononi, na Fiston amefikisha mabao sita.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa