Straika wa Yanga Fiston Mayele amesema kuwa yeye hana tofauti yoyote na kiungo wa timu hiyo Stephen Azizi Ki kama ambavyo alikuwa anasikia baadhi ya minong’ono kwa baadhi ya mashabiki.

Mayele amesema anafahamu kuwa wapo baadhi ya watu wanahisi kwamba yeye na Azizi wanagombea ufalme ndani ya timu hiyo jambo ambalo halina ukweli wowote na haiwezekani ikawa hivyo kato yao.

mayele, Mayele Afunguka Kuwa na Ugomvi na Azizi Ki, Meridianbet

Mayele alikwenda mbali kwa kusema na ndiyo maana hata alipofunga bao Azizi lililowapeleka kwenye makundi ya shirikisho Afrika, alishangalia kama yeye amefunga kwa kuwa wote wanaitakia mafanikio klabu hiyo.

“Mimi sina matatizo na Azizi Ki, maana najua kuwa wapo baadhi ya watu walikuwa wanadhani kuwa nina tofauti naye na kubwa ikiwa ni kugombea ufalme kwenye klabu.

“Sisi wote ni wafanyakazi wa Yanga, mimi nimetoka Congo kuja hapa kufanya kazi na Azizi katoka kwao na kuja kutafuta huku, kwanini tugombane?,” alisema Mayele.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa