Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ameweka wazi kuwa kulikuwa na sababu nyingi sana ambazo zilipelekea wao kupambana na kupata bao la ugenini na la ushindi wakiwa Tunisia na kuwatoa Club Africain.

Mayele alifunguka kuwa moja ya kitu ambacho wao kama wachezaji kilikuwa kinawaumiza ni maneno ya kejeli kutoka kwa mashabiki ambao walikuwa wanasema hawana faida kwenye timu hiyo kwa kuwa wanashinda kufanya vizuri kimataifa.

Mayele, Mayele: Kutukanwa Kulitupa Hasira, Meridianbet

Akizungumza sababu ambayo iliwapa hasira ya kupambana zaidi wakiwa ugenini Mayele alisema: “Tulikuwa tunajisikia vibaya sana kuambiwa kuwa hatuna maana kwenye timu na baadhi ya mashabiki kwa sababu tunashindwa kwenye kimataifa.

“Hayo yalikuwa ni maneno mazito sana kwa kila mchezaji. Tukawa tunaumia sana kusikia maneno hayo na ndiyo maana tukajitoa kwa moyo wote. Mimi nilipotoka nilizoea kucheza mashindano hay ana nilikuwa naumia pia kuona tunatolewa.”

Mayele aliongeza kuwa, mashabiki watarajie kuona timu yao ikifanya vizuri kwenye mashindano hayo baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa