Nyota mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC Fiston Mayere ameteka mitandao ya kijaamii kutokana na tetesi ambazo zimekuwa zikisambazwa kuwa tayari ameshasajiriwa na klabu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini Kaizer Chief.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi zinazothibitisha usajiri wa Mayere kusajiri na klabu ya Kaizer Chief, isipokuwa taarifa za mwandishi kutokea nchini Ghana Nuhu Adams, ambaye aliandika kwenye kurasa zake za kijamii kuwa kaizer Chief wamemsajiri mshambuliaji kutoka Yanga kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Fiston Mayere, Fiston Mayere kweli Asaini Kaizer Chief?, Meridianbet

Mpaka sasa sio Yanga wala kaizer Chief ambazo wametoka kuthibitisha taarifa hizo, klabu ya Kaizer Chief imetangaza usajiri wa Muzi Maluleke, ambaye anaenada kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi wa timu hiyo.

Mkataba wa Fiston Mayere na Yanga umebakia mwaka mmoja, sasa ni wakati wa Yanga kumuongezea mkataba, wamuuze au aondoke huru msimu ujao.

Fiston Mayere ni sehemu ya mafanikio ya Yanga msimu huu, kwani magoli yake 19 na kusaidia kupatikana menginne matano, yameisaidi klabu ya wananchi kumaliza ukame wa miaka minne pasipo ubingwa wowote kwa kuchukua ubingwa ligi kuu ya Tanzania na kuifikisha fainali ya Azam Confideration Cup mwaka huu.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa