Klabu ya Inter Milan imethibitisha kumalizana na klabu ya Chelsea kufanikisha uhamisho wa Romelu Lukaku kwa mkopo wa muda mrefu ambapo kiasi cha  €8.5milioni kimetumika kukamilisha uhamisho huo.

Romelu Lukaku amekubali kupunguza kiasi chake cha mshahara ili aweze kufanikisha uhamisho wa kwenda nchini Italia kwenye klabu ya Inter Milan, ambapo akiwa Chelsea alikuwa anavuna kiasi cha €12milioni.

Inter Milan, Inter Milan Wamalizana na Chelsea kwa Lukaku, Meridianbet

Mwanasheria Sebastien Ledure, ambaye alikuwa anasimamia mazungumzo hayo tangu Lukaku alivyotengana na wakala wake Federico Pastorello, alinukuliwa akisema; “Hakuna aliyeamini ikiwa ingewezekana kwa mara ya kwanza, na walifikili kuwa deal hili halitawezekana.

“Tulifanya kazi chini ya kivuli cha mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea na menejimenti ya Inter Milan. Lukaku kweli anarudi Inter, na nimafanikio. Mara zote nilikuwa nina hofu kuwa mazungumzo yangeweza kushindikana kutokana na ukubwa wa uhamisho uliopita, lakini tulikuwa na imani tangu siku ya kwanza.

“Tulikwenda hatua kwa hatua. Hakuna aliyejua nini kitatokea ndani ya mwaka. Wacha tufurahie kurudi kwake kisha tutaona matokea matokeo mazuri tu kwenye jambo hili.”

Inter Milan wamelipa kiasi cha €8.5milioni, ikiwa watafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Italia serie A, basi itawapasa kuonngeza kiasi cha €4milioni kwenye ada ya uhamisho wake wa mkopo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa