Kocha wa raia wa Afrika Kusini Pitso Mosimane ameweka wazi kuhusu hatma yake ya baadae kwa kusema kuwa atapumzika kwenye kazi ya ukocha na kuwekeza nguvu zake kwenye shule yake.

Pitso Mosimane kwenye kipindi chake cha miaka miwili alichokitumia akiwa na miamba ya Misri Al Ahly, amefanikiwa kushinda makombe matano yakiwemo mawili ya CAF Champions League, Ijapokuwa, kushindwa kwake kuchukua ubingwa wa nchini humo, ulipelekea kukosolewa na wakongwe wa klabu hiyo na wachambuzi wa soka wa Misri.

Pitso Mosimane

 

Pitso Mosimane akizungumza na Kaya959 alinukuliwa akisema; “Nina furaha kupumzika. Nina furaha kuamka saa tano na nina ya furaha yakuwa siwajibiki kwa mtu yoyote kwa muda huu. Nitarudi kwenye kazi ya ukocha pale tu nitakajisikia kuwa nahitaji kurudi.”

Shule ya Pitso Mosimane Soccer Schools, imeanza kufanya kazi ya udahili kwa njia ya mtandao, huku wakitarajia kufunga zoezi la udahili siku ya Ijumaa tarehe 15 July 2022.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa