Yakiwa yamesalia masaa machache kabla ya mchezo wa Simba na Ihefu pale kwa Mkapa Dar, uongozi wa klabu ya Simba umefunguka kuwa timu hiyo haitafungwa tena msimu huu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahemd Ally alisema, timu ambayo inakuwa inawani ubingwa haiwezi kuwa na matokeo ya kupanda na kushuka, kwa maana ya kufungwa, kushinda na kutoka sare, badala yake inatakiwa iwe inavuna alama tatu tu.

simba, Simba Sahau Kufungwa Tena NBC Premier League, Meridianbet

Ahmed alisema, wameshafanya makosa kwenye mechi chache ambazo wamecheza na anatoa kwa ahadi kwa mashabiki wa klabu hiyo kuwa hawataona timu yao ikidondosha alama.

“Najua kuwa inakatisha tamaa kwa timu kama Simba ambayo inagombea ubingwa inakuwa na matokeo ya kupanda na kushuka. Tunatoa ahadi kwa mashabiki wetu kuwa tunakwenda kupambana kwenye kila mchezo.

“Hatutaki kudondosha alama tena kwenye mechi zetu na nawaomba mashabiki waje kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Ihefu kwani uwepo tunahitaji sana,” alisema Ahmed.

Simba wamepoteza mechi na kutoka sare kwenye mechi tatu za ligi hadi sasa, wakiwa wamecheza mechi tisa, wakiwa wamevuna alama 18.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa